WAANZILISHI NA VIONGOZI

Team ya M-kopa ina waasisi na Viongozi wakubwa waliopata waliopata tuzo za Huduma ya M-Pesa kutoka Vodafone na Safaricom wafanyakazi wakenya na wakimataifa wenye ujuzi wa kina katika Uinjinia wa program , Ugavi , Fedha na Huduma kwa wateja


Anne

ANNE CHEGE MWAURA

Mkuu wa kitengo cha Utawala

Anne alijiuinga na M-kopa kutoka mwaka 2011 ,kabla ya hapo alifanya kazi na Deutsche Bank, CARE Kenya na Mobile Ventures Kenya na alifanya kazi katika kitengo cha Huduma kwa wateja na I.C.T , Anna ana Shahada ya Sanaa ya Utawala wa Biashara kutoka (B.A)chuo cha Gosheni na uzoefu wa miaka 10 katika uongozi na huduma za kiufundi


Chad

CHAD LARSON

Mkurugenzi wa Fedha / Mhasisi

Chad ni mmoja kati ya waasisi wa M-kopa ambaye alikuwa Afisa mkuu wa fedha Mecene Investment , Meneja wa mfuko wa Africap Microfinance Investment Fund huko Johannesburg Chad ni mwanachama wa CFA charterholder na ana Shahada ya Uzamili kutoka chuo kikuu cha Oxford na uzoefu wa uwekezaji wa kibenki kwa miaka 10 alioupata Benki ya Marekani


Edwin

EDWIN KADUKI

Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia

Edwini alijiunga na M-Kopa mwaka 2011 tokea Knowing Ltd Nairobi kampuni ya kikenya ya kutengeneza programu na mifumo ya Kibenki , biashara na Serikali kama mshauri mwandamizi wa mifumo , Edwini ana uzoefu wa Zaidi ya miaka 13 katika ufumbuzi ,kutengenezaji waprogramu na mifumo ya kibiashara


Jesse

JESSE MOORE

Mkurugenzi mkuu /Muhasisi/span>

Jesse Moore ana uzoefu wa Zaidi ya miaka 10 katika fani ya kuendeleza Ubia wa Masoko ya Teknologia kabla ya kuwa Mwanzilishi wa M-Kopa , Jese alikuwa Mkurugenzi mkuu mtendaji katika kampuni ya Signal Point Partners na GSMA Development Fund , Jese ana Shahada ya Uzamili kutoka chuo kikuu cha Oxford University (Skoll Scholar) na shahada ya Sanaa ya Uongozi kutoka UNC Chapel Hill (Morehead Scholar).


June

JUNE MULI

Mkuu wa Huduma kwa wateja

June ana Uzoefu wa Huduma kwa wateja wa zaidi ya miaka sita alijiunga na M-kopa mwanzoni mwa mwaka 2012 akitokea Vodafone(UK) , GTV, Multichoice Kenya and SMART TV ,June ana cheti cha Uzamili katika fani ya Fedha na Uchumi kutoka chuo kikuu cha Middlesex University Business School na Shahada ya Sanaa ya Benki na fedha ya chuo kikuu cha Maseno


Nick

NICK HUGHES

Mkurugenzi wa Mipango / Mhasisi

Nick ni muingizaji na mpangiliaji wa bidhaa mpya ya M-kopa katika soko Jipya , kabla ya hapo alikuwa ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Signal Point Partners , Mshauri mwanzilishi wa M-kopa , mpaka 2009 Nick alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Malipo cha kimataifa cha Makampuni ya Vodafone ndie alieanzisha M-pesa 2014 , Nick ana Shahada ya Uzanifu ya Matumizi ya Sayansi , shahada ya Uzamili kutoka London Business School , mwaka 2010 alipata Tuzo ya ubunifu ya Uchumi


Pauline

PAULINE VAUGHAN

Mkurugenzi wa Uendeshaji
Pauline alijiunga na M-kopa mapema mwaka 2012 akitokea safaricom na kuleta Ujuzi na ubunifu wake wa teknologia ya simu , Pauline alifnya kazi Safaricom kwa miaka 10 na miaka 4 katika M-peas timu ya uongozi M-pesa , Pauline ni mzaliwa wa kenya mwenye hari ya kuona wakenya wanaishi maisha mazuri Pauline ana Shahada ya Uinginia wa Ujenzi kutoka chuo kikuu cha Cape Town