M-KOPA SOLAR ZINAUZWA WAPI?

M-KOPA Solar zinapatikana popote nchini kwenye vodashop zilizoorodheshwa na kwa mawakala wetu  waliosajiliwa kwa maelezo zaidi piga number  0764701100 au tembelea Vodashop zilizoorodheshwa.


NINI KINAHITAJIKA MTU KUWA MTEJA WA M-KOPA?

Wakala wetu atakupa maelekezo kuhusu namna ya kufanya malipo ya bidhaa yetu na baada ya usajili utapokea simu kutoka M-KOPA huduma kwa wateja na utapewa maelezo kuhusiana na hatua inayofuata, ili kusajisajiliwa  unahitaji kuwa na kitambulisho na simu iliyosajiliwa kwa M-pesa.


NINI KITAFATA BAADA YA KUMALIZA MALIPO?

Baada ya kumaliza malipo ya kifaa chako utakuwa mmiliki kamili wa kifaa chako utakitumia bila kulipia tena.


JE NAWEZA KUMNUNULIA KIFAA CHA M-KOPA MTU YEYOTE?

Ndio unaweza kumnunulia kifaa cha M-KOPA Solar mtu yeyote kwa maelezo zaidi piga simu huduma kwa wateja  0764701100.


JE NAHITAJI FUNDI KUFUNGA KIFAA CHA M-KOPA SOLAR NYUMBANI KWANGU?

Hapana ni rahisi na kwa wepesi zaidi  unaweza  kufunga kifaa cha M-KOPA Solar nyumbani kwako, weka Solar Panel yako juu ya bati na betri yako ndani ya nyumba maali palipo Salama na unganisha  taa na vifaa vingine kwenye betri kwa urahisi zaidi , kifaa cha M-KOPA solar kinatoa mwangaza wa kutosha na ni rahisi kuhamishika, kwa maelezo zaidi piga 0764701100 huduma kwa wateja kwa msaada zaidi.


NITAFANYA NINI KAMA KIFAA CHANGU HAKIFANYI KAZI?

Tafadhali hakikisha kuwa kifaa chako kina salio na kinaingiza moto /charge, kama tatizo linaendelea  tafadhali piga huduma kwa wateja 0800756666 kwa msaada zaidi.


KUNA DHAMANA KWENYE KIFAA CHA HOME SOLAR SYSTEM?

Ndio, dhamana lakini hutegemea na aina ya kifaa ulichonunua, tafadhali angalia ukurasa ili kupata maelezo zaidi kuhusu dhamana.


JE, M-KOPA INA SOLAR PANEL INAYOWEZA KUWASHA TELEVISHENI?

Kwa sasa tunaanda bidhaa mpya na za kusisimua na tutawataarifu punde zitakapokuwa tayari , tafadhali kamilisha malipo ya kifaa chako ili uwe katika nafasi nzuri ya kupata bidhaa zifuatazo.


NAWEZAJE KUWA WAKALA WA M-KOPA?

Kama unataka kuwa wakala wa M-KOPA, tafadhali  wasiliana  kupitia barua pepe:- dealer@m-kopa.com  kwa maelezo zaidi