M-KOPA ilitambuliwa kati ya makampuni bora 100 ya kimataifa rafiki kwa Mazingira kwenye kongamano la tuzo za 100 Global Cleantech ambapo iliwakilishwa kwa mchango wake wa mawazo na Ubunifu wenye matumaini ya kuleta Ufumbuzi wa maswala ya Usafi wa mazingira siku za usoni.                                                                                                                                                                                                                                                                 M-KOPA Solar inaongoza katika soko la Nairobi kwa kutoa huduma za Nishati kwa mfumo wa kulipia kadri utumiapo kwa wateja ambao makazi yao hayajaonganishwa na Gridi ya taifa , Ndani ya miaka miwili ya kibiashara tumeweza kuonganisha makazi Zaidi ya 100,000 Afrika Mashariki kwenye nishati bora na nafuu ya mwanga wa Jua kwa kufanya malipo kwa kutumia mtandao wa simu , kwa mwezi mmoja tuu M-KOPA Solar imeokoa garama za zaidi ya masaa milioni 12.5 ya matumizi ya mafuta ya taa kwa kutoa mwangaza bure , kwa ujumla M-KOPA Solar imeokoa garama ya Zaidi ya Dola za kimarekani milion 75 kwa makadirio ya kuokoa Dola 750 kwa kaya moja ukilinganisha na matumizi ya kipindi cha mafuta ya taa kwa miaka minne.

Jese Moore mhasisi na mkurugenzi wa M-kopa solar amesema M-kopa iliandaliwa kama tekinolojia mbadala ya malipo kwa simu , kwa kuona kuwa kuna uwezekano wa kuhamisha kiwango kidogo cha pesa kwa gharama ndogo na kuleta mapinduzi na katika matumizi ya Nishati , kwa sasa tunatoa huduma ya hali ya juu ya nishati ya Jua kwa kukusanya malipo kidogo kidogo kutoka kwa wateja kwa wao kuchagua kiasi wa wakati wa kufanya malipo.

Global Cleantech 100 inaangalia kwa kina Makampuni binafsi yenye uwezo wa kufanya mabadiliko ya makubwa katika Masoko , hii inapangwa kwa kulinganisha jumuisho la takwimu za utafiti za Clean Group kwa kulinganisha na kutoa uamuzi wa mamia ya Mapendekezo , kuna jopo la wataalamu 84 waliochaguliwa kutoka kwa waekezaji na makampuni ya kimataifa kutoka makampuni mbalimbali ya kimataifa ya utafiti na ubunifu wa tekinolojia kutoka Asia , Ulaya na Amerika ya kaskazini.

The Global Cleantech 100 inawakilisha na kutoa msukumo kwa wajasiriamali kuelekea Cleantech space ambayo inatokipaombele kwenye ubunifu , alisema Sheeraz Haji, Cleantech Group’s CEO Kwa mwaka huu walipokea nukuu za mapendekezo yenye idadi ya makampuni   tofauti 5,995 kutoka mataifa 60 yaliyoshiriki na kufanyika mchujo wa makampuni 327 uliopitiwa na wataalamu wa Cleantech Group’s na baadae kupatikana makampuni 100 kutoka nchi 17.